Msuva aipa matumaini ya ushindi Difaa

Muktasari:

Katika michuano hiyo ya  Moroccan Throne Cup, Difaâ ilitoshana nguvu na  Ittihad kwenye mchezo wa awali kwa kutoka sare ya bila kufungana.

Dar es Salaam.  Timu ya Difaâ Hassani d'el-Jadida anayoichezea  mshambuliaji wa Kitanzania  Simon Msuva,  inasafiri leo kutoka  El Jadida kuelekea Tangier kucheza mchezo wa marudiano na Ittihad Tanger, Jumatano.
Katika michuano hiyo ya  Moroccan Throne Cup, Difaâ ilitoshana nguvu na  Ittihad kwenye mchezo wa awali kwa kutoka sare ya bila kufungana.
Msuva amesema kuwa nia yao ni kusonga mbele kwa hiyo wamejipanga kwenda kupata matokeo ya ushindi ugenini.
“Hakuna kinachoshindikana kwenye mpira, kama wao walivyoweza kupata sare ndivyo na sisi tutakavyo pata matokeo ya ushindi ugenini,” alisema Msuva.