Mshambuliaji wa Cystal Palace akerwa mashabiki wabaguzi

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alituma kwenye ukurasa wake wa Istagram akiwalaumu mashabiki wa Manchester United na Liverpool kutokanana tabia ya kumuita nyani mweusi.

Mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha amesema anachukizwa na mashabiki wa Manchester United na Liverpool ambao humuita ‘nyani mweusi’ wanapomtumia ujumbe mfupi kwenye mitandao ya kijamii.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alituma kwenye ukurasa wake wa Istagram akiwalaumu mashabiki wa Manchester United na Liverpool kutokanana tabia ya kumuita nyani mweusi.

Alisema tabia hiyo humkwaza na huenda wamekuwa na lengo la kumharibia siku. Awali, Zaha alisajiliwa Manchester United mwaka 2013.

Kocha wa klabu hiyo, Frank de Boer alithibitisha kuwa mchezaji huyo ni kweli amekuwa akitukanwa.