Mrundi wa Simba anarudi tena

Wednesday June 13 2018

 

By DORIS MALIYAGA

BEKI wa zamani wa Simba, Emery Nimubona anajua sasa ni kipindi cha usajili kwenye ligi ya Tanzania ameanza michakato ya kuhakikiasha anarudi Bongo.
Nimubona amesema anatamani kurudi na kuna baadhi ya timu ameanza kufanya nazo mazungumzo ya awali.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Vital 'O' ya nchini kwao Burundi  amesema, pamoja na kucheza nyumbani kwao hamu yake ni kurudi Tanzania.
"Nimekuwa Tanzania kwa kipindi, nimeishi vizuri na nafurahia maisha huko nafikiri haya mambo yakienda sawa nitakuja huko na waambie timu nyingine kama tunaweza kukubaliana,"alisema Nimubona.
Hata hivyo, Nimubona hakutaka kuweka wazi ni timu gani zinazomuhitaji ingawa awali alizitaja Mbeya City na Stand United.