Mpinzani wa Yanga wakimataifa aburuzwa Ethiopia

Dar es Salaam. Baada ya jana Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kupangiwa kucheza na timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia, imebainika timu hiyo ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ethiopia.

Welayta ambayo hadi sasa imecheza michezo 15 imevuna pointi 19 na kuifanya kusimama nafasi ya nane  jambo ambalo linaipa matumaini makubwa Yanga kufanya vyema kwenye mashindano hayo.

Dedebit inaongoza msimamo wa Ligi hiyo ikiwa imeshacheza michezo 15 na kujizoea pointi 29.

Mchezo wa awali unatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 6 na 8 Aprili na marudiano yamepangwa kuwa Aprili 17 hadi 18 mwaka huu.