Mpasuko! Huko Argentina sio salama

Muktasari:

  • Ni hivi, baada ya kushuhudia mwenendo mbovu wa timu yao kwenye muhuano ya Kombe la Dunia inayoendelea kutimua vumbi, mastaa walimshauri Sampaoli kuhusu upabgaji wa kikosi hasa kuelekea mechi ya pili, lakini Kocha huyo hakutaka kushauriwa. Akafanya yake.

Moscow, Russia. Huko Argentina unaambiwa mambo hayako sawa. Kumewaka moto ile mbaya. Wachezaji wameliamsha balaa. Mastaa wote kwenye kikosi wamjia juu Kocha, hawamtaki Jorge Sampaoli unaambiwa. Ni kubaya!

Ni hivi, baada ya kushuhudia mwenendo mbovu wa timu yao kwenye muhuano ya Kombe la Dunia inayoendelea kutimua vumbi, mastaa walimshauri Sampaoli kuhusu upabgaji wa kikosi hasa kuelekea mechi ya pili, lakini Kocha huyo hakutaka kushauriwa. Akafanya yake.

Taarifa zinasema kwamba, wachezaji wa Argentina wakiongozwa na Nahodha wao Lionel Messi, walishauri kuwe na beki imara ya watu wanne, kwa ajili ya ulinzi lakini Sampaoli akaamua kutumia mabeki watatu, mwisho wa Sikh ndio kama mlivyosikia. Walipigwa 3-0 na Croatia.

Baada ya kuona hawasikilizwi, wachezaji wa Argentina wameamua kuntimua Sampaoli. Ni kwamba, juzi, Ijumaa wakiongozwa na Javier Mascherano, wachezaji hao, waliitisha kikao na Rais wa Shirikisho la soka la Argentina, Claudio Tapia, Sampaoli na bencbi lote la ufundi.

Katika kikao hicho, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli waliyofikia, wachezaji walishinikiza kung'atuka kwa Sampaoli na benchi lake huku ikidaiwa kuwa wachzaji wanamtaka nyota wa zamani wa Argentina, Jorge Barruchaga, aliyekuwa katika kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1986, kukabidhiwa timu.

Hata hivyo, baada ya mazungumzo ya takribani masaa mawili, zoezi la kumtimua Sampaoli ambaye aliwahi kuifundisha Chile kwa mafanikio makubwa ilishindikana na inadaiwa kuwa, wachezaji hao wamemwambia kama anataka kukaa kwenye benchi la ufundi au kuondoka ni hiyari yake, ila wao hawamtambui.

Kwa mujibu wa Ricardo Giusti ambaye ni mtu wa karibu na Burrachaga, ni kwamba mastaa hao wamemtaka Sampaoli kutojihusisha na upangaji wa kikosi kwani kazi hiyo wataifanya wao kabla ya kuwavaa Nigeria katika mchezo wa mwisho wa makundi, utakaopigwa siku ya Jumatano, mjini St. Petersburg.

“Wachezaji wanataka kujenga timu, wamewaambia Sampaoli na Tapia kuwa watapanga kikosi kitachoivaa Nigeria wenyewe, hawamuhitaji Sampaoli, hawana imani naye tena. Sampaoli ameambia akipenda kubaki sawa, akitaka kwenda pia ni sawa, ila jukumu la kuamua nani acheze sio lake tena," alisema Giusti.

Inadaiwa kuwa, baada ya kipigo cha 3-0, Mascherano na Christian Pavon, walizinguana na baada ya Mascherano kumlaumu Willy Caballero, ambaye alifanya uzembe uliozaa bao la kwanza.

Argentina ambayo ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali, kwenye michuano ya Kombe la Dunia, yaliyofanyika Brazil mwaka 2014, walipata matumaini ya kuendelea kubakia nchini Russia baada ya Nigeria kuitungua Iceland na sasa watahitaji tu kuifunga Nigeria ili waweze kusonga mbele katika hatua inayofuata ya 16 bora.