Mourinho aanza tambo, ajibu mapigo

Muktasari:

Man United jana usiku ilitinga fainali ya Kombe la FA kibabe kwa kuichapa Tottenham Hotspurs mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wambley, jijini London.

KOCHA Jose Mourinho amewauliza mashabiki waliokuwa wakimponda kama wana maswali, baada ya kikosi chake cha Manchester United kutinga fainali ya Kombe la FA.

Man United jana usiku ilifuzu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham kwenye Uwanja wa Wambley, jijini London.

Mourinho amesifu kazi nzuri ya wachezaji kwa kuonyesha morali ya kupambana uwanjani huku akiwapiga kijembe waliokuwa wakikiponda kikosi chake kuwa hakichezi soka lenye ubora.

“Tunapaswa kujiuliza kwanini wamekuwa wakituponda wakati tutacheza kwa kiwango bora dhidi ya timu zote. Tunastahili,” anasema Mourinho.

Katika mchezo dhidi ya Spurs, mshambuliaji nyota wa zamani wa Arsenal, Alexis Sanchez alisawazisha bao la Dele Alli kisha akapika lingine la ushindi kwa Ander Herrara.