Moore aiongoza West dhidi ya East ushindi wa 130-121

Muktasari:

  • Wakongwe wa West waliibuka na ushindi kwenye mchezo huo baada ya kuonyesha umahili katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali.

Marekani. Maya Moore wa timu West amefanikiwa kufunga pointi 23 kwenye mechi iliyowakutanisha wakali wa kikapu wanawake ‘WNBA ALL –Star’ huku naye Nneka Ogwumike akifunga pointi 22 na kufanya matokeo kuwa 130-121 dhidi ya East mchezo uliopigwa jana Jumamosi.

Wakongwe wa West waliibuka na ushindi kwenye mchezo huo baada ya kuonyesha umahili katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali.

Moore alifunga mara tisa katika nafasi 17 alizopata. Mchezaji huyo alitangazwa kuwa nyota wa mchezo huo.