Mo awapa mbinu Yanga

Muktasari:

  • Mo Dewji kupitia mtandao wa Twitter ameeleza hisia zake kufuatia migogoro na hali ambayo wanapitia hivi sasa pale Jangwani amewataka  Yanga  kunyanyuka  na kuungana kipindi hiki.

Dar es Salaam. Wahenga wanasema ‘ adui muombe njaa…’ lakini mambo yamekuwa tofauti kwa shabiki na mwekezaji mkubwa wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ akiomba watani zake wajadi Yanga kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wanachopita.
Yanga inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo juu ya mikataba ya baadhi ya wachezaji, uongozi pamoja na ukata wa fedha unaowakumba katika klabu hiyo
Mo Dewji kupitia mtandao wa Twitter ameeleza hisia zake kufuatia migogoro na hali ambayo wanapitia hivi sasa pale Jangwani amewataka  Yanga  kunyanyuka  na kuungana kipindi hiki.
“We need a strong Yanga for Simba to excel. We need a strong Yanga for a better Taifa stars. I pray that young africans get through these difficult times. They need to be calm and regroup.”
“Tunahitaji Yanga imara ili Simba iweze kuendelea. Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya.”