Mo Salah amponza bilionea wa Makkah

HUKU ukiwa ni mwezi mtukufu wa Ramadhan, tajiri mmoja wa Saudi Arabia amekumbana na pingamizi kali baada ya kuweka wazi nia yake ya kutaka kumzawadia staa wa Liverpool, Mohammed Salah na kipisi cha uwanja mjini Makkah.

Makkah ni mji mtakatifu kwa waumini wa Kiislamuu ambako waumini wa dini hiyo kote duniani husafiri kwenda kuhiji (kusujudu) kipindi cha mfungo.

Kutokana na utukufu wa mji huo, shamba hairuhusiwi kuuziwa mtu yeyote haswa kama sio raia wa Saudi Arabia.

Sheria hiyo ndio ilimweka kikaangoni Naibu Mwenyekiti wa Manispaa ya Makkah, Fahd Al-Rouqi kwa hatua yake ya kutaka kumpa Salah kipande cha uwanja wake mjini humo ili aweze kuuza na kuwasaidia maskini au ajengee msikiti.

Hatua hiyo imetokana na Al-Rouqi kufurahishwa na tabia za Salah kwa kunga’aa Ligi Kuu England msimu huu, pamoja na kuonyesha kuonea fahari dini yake ya Kiisalamu na kusaidia maskini nchini kwao Misri.

Hata hivyo, alipata upinzani mkali kutoka kwa mashabiki na waumini wengi wa Kiislamu waliomtaka Al-Rouqi kujifanya mpuzi wa kutoielewa sheria inayomzuia raia wa nje kumiliki shamba Saudia na hasa Makkah.

Wengi walionyesha kukerwa kwao kwenye mtandao wa Twitter walikotupia hasira zao juu ya kigogo huyo.