Mo Ibrahim unatania au?

KIUNGO wa Simba, Ibrahim Mohammed 'Mo Ibrahim' amesema, habari za kwake kujiunga na Yanga ni stori tu, yeye hana hata mpango wa kwenda huko.

Mo Ibrahim ambaye hakuwa kwenye wakati mzuri ndani ya kikosi chake kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kifamilia.

Amesema, anasikia tetesi hizo  kama  watu wengine lakini kwa sababu yeye ndiyo muhusika, ameamua kutoa la moyoni na kusema, hakuna kitu kama hicho.

"Hakuna mpango huo, mimi ni mchezaji wa Simba achana na habari za Yanga. Sijui chochote na mimi nasikia tu kama wewe unavyosikia, watu wanapenda kuzungumza sana sijui kwa nini,"alisema Mo Ibrahim ambaye baada ya kuulizwa kama alishapigiwa simu na viongozi wa Yanga, Mo hakutaka kufunguka kwa undani akabaki amenyamaza tu.