Mngeta Rangers, City Boys zafanya kweli

Muktasari:

  •  Mshambuliaji wa Mngeta Rangers FC, Juma Ally alikuwa mwiba mchungu kwa Bodaboda Itongoa FC kwa kufunga mabao tatu pekee yake dakika ya 20, 28 na 44 wakati Samuel Mwamwezi alifunga bao la nne dakika 75 na Levocatus Mwenda akihitimisha kwa bao la tano dakika ya 81

Mngeta Rangers FC imeanza kwa  kishindo mashindano ya Rwakatare Cup 2017 baada ya kuisambaratisha Bodaboda Itongoa  FC kwa mabao 5-1 katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo.

 Mshambuliaji wa Mngeta Rangers FC, Juma Ally alikuwa mwiba mchungu kwa Bodaboda Itongoa FC kwa kufunga mabao tatu pekee yake dakika ya 20, 28 na 44 wakati Samuel Mwamwezi alifunga bao la nne dakika 75 na Levocatus Mwenda akihitimisha kwa bao la tano dakika ya 81.

Mshambuliaji, Maisha Muhumbaki alifunga bao la kufutia machozi kwa Bodaboda Itongoa FC dakika ya 45.

Katika mchezo mwingine City Boys ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Home Sport Club na kuwaondoa mashindano.

Mabao ya City Boys FC yalifungwa na Jafari Macheka dakika ya 26, Mboma Mboma dakika ya 57, Rustic Makero alihitimisha kwa kufunga bao la tatu dakika ya 60.

Mbasa FC ilitupwa nje mashindano kwa mikwaju ya penalti 8-7, baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Muungano FC iliyosonga mbele.