Mkwanja wa SportPesa wafufua matumaini Polisi

Monday September 11 2017

 

By Imani Makongoro

Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa imeipa timu ya Polisi Tanzania kitita cha Sh20 milioni na vifaa vya michezo kwa ajili ya ushiriki wao kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza.

Polisi FC itafungua dimba Septemba 17 dhidi ya JKT Mlale mjini Songea.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro alisema msaada huo umewaongezea morali ya ushindani kwenye ligi hiyo na iiwezekana kupanda daraja.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema wameisapoti timu hiyo kutokana na mchango wake kwa jamii.