Mourinho kumpiga bei Mkhitaryan

Muktasari:

Ozil amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United katika usajili wa dirisha dogo au majira ya kiangazi baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

London, England. Jose Mourinho anafirikia kufanya uamuzi mgumu wa kumpiga bei mchezaji wake kiungo Henrikh Mkhitaryan ili kutoa nafasi kwa Mesut Ozil.

Ozil amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United katika usajili wa dirisha dogo au majira ya kiangazi baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mourinho anataka kumpunguza kiungo huyo mshambuliaji ili kutoa nafasi kwa Ozil ambaye amekuwa kipenzi chake tangu wakiwa Real Madrid.

Mjerumani huyo amegoma kutia saini mkataba mpya licha ya kupandiwa dau la mshahara na klabu yake ya Arsenal iliyoweka  mezani Pauni 235,000. Awali, Ozil alitaka Pauni 300,000 kwa wiki.

“Nina mabeki wawili,nina Ashley Young anayeweza kucheza pia winga. Viungo Ander Herrera, Zlatan Ibrahimovic, Marcus Rashford ni straika lakini unapokuwa na Mkhitaryan sidhani kama unaweza kuwa naye,” alisema Mourinho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Armenia amecheza dakika 19 tu katika kikosi kilichoanza tangu Novemba 5 licha ya kuonyesha kiwango bora, lakini amekosa mvuo kwa bosi huyo.