Mkali wa Bollywood kushiriki tuzo za Azam za SZIFF

Preetika Rao (Aliyah)

Dar es Salaam. Mkali wa Filamu nchini India, Preetika Rao (Aliyah) anatarajiwa kutua nchini kushiriki katika hafla ya tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zinazoendeshwa na Azam Media.

 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alisema, tuzo hizo zitafanyika Aprili Mosi kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Aliyah ni staa wa tamthili ya Beitehaa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

 

"Tuzo zitakuwa na vipengere 18, pia kuna tuzo nyingine ya 19 itakayotolewa kwenye kipengere cha Chaguo la mtazamaji," alisema Tido na kuendelea.

 

"Zoezi linaloendelea sasa ni upigaji wa kura ya tuzo ya chaguo la mtazamaji kwenye filamu zilizochaguliwa kwa kuandika neno Ndiyo na kuandika kodi ya filamu ambayo iko kwenye kava la filamu huska na kuituma kwenda namba 0757339567," alisema Tido.

 

Alisema filamu 143 zilipambanishwa ili kupata zile za kuingia kwenye tuzo ambazo zilionyeshwa kwenye chaneli ya Sinema Zetu katika king'amuzi cha Azam Tv.

 

"Hivi ni tuzo Kubwa za kimataifa ambazo zitashindanisha filamu Kali za lugha ya kiswahili za wasanii tofauti  wa Afrika Mashariki," alisema Tido.

 

Alisema watu maarufu nchini na nje ya nchi wamealikwa kushiriki tuzo hizo zitakazorushwa live simu hiyo.