Mgombea achemka kujibu swali

Saturday August 12 2017

 

By Matereka Jalilu

Dodoma. Mgombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda ya sita yenye mikoa ya Katavi na Rukwa, Baraka Mazengo ameshindwa kujibu swali aliloulizwa na mpiga kura baada ya kujinadi.

Mazengo alijinadi kwa kuomba kura na kwamba ataiwakilisha mikoa hiyo vyema endapo watamchagua na kumpa ridhaa ya kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF, lakini swali aliloulizwa lenye majibu manne alishindwa kujibu yote na kukiri kwamba hafahamu.

Mjumbe huyo alimuuliza mgombea kwamba awatajie vyama vinne vilivyomo kwenye mikoa hiyo ambapo alijibu vyama viwili pekee vya Mpanda na Katavi.

Mazengo alishindwa kujibu vyama viwili vingine na kuwaacha wajumbe wakimshangaa kwamba anakwenda kuongoza nini wakati hajui hata vyama vya wilaya vya kanda yake.