Mfumo 3-4-3 waibeba Mbao FC

Muktasari:

  • Mbao ni imekuwa ikitumia mfumo 3-4-3 na kuwapata mafanikio katika msimu uliopita na msimu huu baada ya kuilazimisha Simba sare ya mabao 2-2 wiki iliyopita.

Beki wa Mbao FC, Sadala Mohammed (19) amesema anaufurahia mfumo mpya wanaoutumia wa walinzi watatu nyuma, viungo wanne na washambuliaji watatu.

Mbao ni imekuwa ikitumia mfumo 3-4-3 na kuwapata mafanikio katika msimu uliopita na msimu huu baada ya kuilazimisha Simba sare ya mabao 2-2 wiki iliyopita.

 “Tupo mimi, Yusuph Mgeta na Yusuph Ndikumana ambao tunacheza nyuma, mfumo ni mzuri na unatufanya tuwe na uwiano mzuri kwenye kuzuia na kushambulia,”

“Huu mfumo wa mabeki watatu nyuma huongezeka na kufikia walinzi watano kwa maana ya mawinga wote wa kushoto na kulia hushuka na kuongeza nguvu kwenye ulinzi.” alisema Sadala.

Hata hivyo Sadala ni zao la Azam ambalo limebadilishiwa majukumu na kocha wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije kutoka  ushambuliaji mpaka kuwa mlinzi wa kati.