Messi ni 'Hat Trick' tu Ulaya!

Muktasari:

Messi sasa anashikilia nafasi ya tatu kati ya washambuliaji waliozifunga timu nyingi tofauti barani Ulaya 'hat trick' ikiwa ni 30. Nafasi ya pili inashikiliwa na Cristiano Ronaldo timu 32, na kinara wao ni Raul aliyezifunga timu 33 tofauti.

Barcelona, Hispania. Mshambuliaji mahiri na nahodha wa Barcelona, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya jana Jumanne kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.

Mabao hayo aliyafunga katika mechi ya kwanza ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV  Eindhoven ya Uholanzi, yamemfanya Messi raia wa Argentina kuwa mchezaji anayeongoza barani Ulaya kwa kufunga 'hat trick' nyingi zaidi ya wengine.

Mchezaji huyo alianza kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa faulo ‘free-kick’ dakika ya 31, ikiwa ni faulo ya nane kwake kufunga kwa mwaka 2018, kabla ya kukamilisha 'hat-trick' ya 42, kwa Barcelona dakika za 77 na 87, ikiwa ni ya nane kwake kwenye michuano ya Ulaya, sita alizifunga kwenye timu ya Taifa ya Argentina.

Aidha Messi ameweza kuifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Raul kwa kufunga mabao 104 katika michuano ya Ulaya akiwa ameyafunga katika michuano 14 tofauti.

Ushindi huo umeiwezesha Barcelona kushinda mchezo wa 25 kati ya 27 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, wamepoteza mechi mbili pekee mchezo wa mwisho kufungwa kwenye uwanja huo ulifanyika Mei, 2013, walipofungwa na Bayern Munich mabao 3-0.

Bao jingine la Barcelona katika mchezo wa juzi lilifungwa na winga wao kutoka Ufaransa, Ousmane Dembele, wakati mlinzi Samuel Umtiti alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mchezo mbaya.

Katika mechi zijazo PSV inayonolewa na kiungo wa zamani wa Barcelona, Mark van Bommel, itaikaribisha Inter Milan ya Italia wakati Barcelona itasafiri kuifuata Tottenham.

, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.