Ni Messi na wenzake 10

Muktasari:

Nyota huyo wa Argentina anashikiria rekodi ya kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mara tano

Barcelona, Hispania. Umekuwa mwanzo mzuri wa msimu 2017/18 kwa Lionel Messi, kuiongoza Argentina kufuzu kwa Kombe la Dunia na pamoja na kuiweka Barcelona kileleni mwa LaLiga akiwa amecheza mechi zote.

Messi amecheza kila mechi msimu huu ikiwa ni dakika 1,350 akiwa na kikosi cha Barcelona na Argentina.

Akiwa amecheza mechi mbili za Supercopa de Espana, mechi saba za ligi, mbili za Ligi ya Mabingwa na nne za kufuzu kwa Kombe la Dunia, Messi amekuwa akijituma zaidi.

Hakuna mchezaji wa Ulaya aliyefikia mafanikio ya Messi, aliyekuwa akimkaribia ni Dani Carvajal aliyecheza dakika 990 kabla ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo yanayomlazimisha kuondolewa katika kikosi cha Real Madrid.

Kwa Messi dakika 990 amezipata katika klabu yake na wiki hii ataziongeza wakati Barca dhidi ya Atletico Madrid ni mchezo kocha wake Ernesto Valverde hawezi kuthubutu kumweka nje.

Ni wazi, Messi mwenyewe ndiye aliyesema hataki kupumzika na anajua jinsi gani atakavyoweza kutunza nguvu zake.