Mchizi kavuta bajaji SportPesa na faida juu

Muktasari:

  • Mshindi huyo alisema kabla ya kutajirishwa na kampuni hiyo ya kiubashiri, alikuwa anafanya shughuli zake kwa kuungaunga hapa mjini, lakini ushindi wake kupitia SportPesa ulibadili mwelekeo wa maisha yake.

MKAZI wa Yombo Vituka jijini Dar es Salaam, Hamis Saleh kama masihara anamiliki Bajaji huku akiwa amevuta mkwanja mwingine wa maana kutoka SportPesa baada ya kubashiri michezo ya soka.

Saleh amesema hakutarajia kama angemiliki chombo hicho kitakachokuwa kikimuingizia noti kama sio kushiriki kwake promosheni za SportPesa.

Mshindi huyo alisema kabla ya kutajirishwa na kampuni hiyo ya kiubashiri, alikuwa anafanya shughuli zake kwa kuungaunga hapa mjini, lakini ushindi wake kupitia SportPesa ulibadili mwelekeo wa maisha yake.

Alisema baada ya kujishindia bajaj mpya na SportPesa ameweza pia kununua pikipiki mbili maarufu kama bodaboda ambazo zinamwingizia fedha kila siku.

Kwa upande wa familia, Saleh alisema mambo yamebadilika sana kwani Bajaj imeifanya familia yake kuishi kwa furaha na uhakika baada ya kupata mradi huo ambao umebadilisha kwa kiasi kikubwa maisha yake.