Mchongo wa SportPesa, Everton

Muktasari:

Kampuni ya SportPesa inayoidhamini klabu hiyo pamoja na Everton zimekuwa zikikusanya jezi zinatolewa na mashabiki, wachezaji na wadau wengine wakati wa mechi za nyumbani kwa Agosti na Septemba na watazingawa Afrika kwa timu ambazo hazina uwezo pamoja na kwa watu binafsi wanaopenda soka.

EVERTON jioni hii watavaana na West Ham United katika mechi yao ya Ligi Kuu England, wakiwa na uzi wenye nembo mpya ya Kits For Africa, kisha kukusanya kwa ajili ya kuzigawa Afrika katika kampeni yao ya kuhamisha soka.

Kampuni ya SportPesa inayoidhamini klabu hiyo pamoja na Everton zimekuwa zikikusanya jezi zinatolewa na mashabiki, wachezaji na wadau wengine wakati wa mechi za nyumbani kwa Agosti na Septemba na watazingawa Afrika kwa timu ambazo hazina uwezo pamoja na kwa watu binafsi wanaopenda soka.

Mechi ya leo Jumapili dhidi ya West Ham chini Kocha Manuel Pellegrini ndio fursa ya mwisho kwa mashabiki kutoa jezi zao na mashabiki wanaombwa kuleta jezi za zamani au vile ambazo hazijatumikwa na kuziweka kwenye eneo la Fan Zone ambalo limeandikwa ‘Kits For Afrika’ ambazo kuziweka kwenye moja ya stoo za Everton.

Kits For Afrika (K4A) ni kampeini inayoendelea ya SportPesa yenye nia ya kukuza soka Afrika kuanzia ngazi ya chini kwenye nchi ambazo SportPesa inafanya kazi tangu kuanzisha kwa kampuni hiyo 2014.