Mchezaji kinda wa Kibongo atua Hispania

Wednesday September 13 2017

 

By Eliya Solomon

Mchezaji kinda wa Kitanzania , Prince Leonard (17) amepata nafasi ya  kwenda  kujiunga na kituo cha Mallorca Toppfotball kilichopo nchini Hispania kwa ajili ya kuendelezwa kisoka.

Kituo hicho cha kibiashara kina wachezaji kadhaa ambao kimewauza kwenye timu kama  Molde, Rosenborg, Brann, Strømsgodset, Sogndal, Assane, Torslanda, Sandnes Ulf, Drexel Dragons, Sandefjord na Bryne.

“Mzee wangu ananisapoti kwa kiasi kikubwa, muda mrefu kidogo nilimweleza kuwa nahitaji kuyatengeneza maisha yangu kupitia mpira. Safari yangu ni mwezi ujao,” alisema Prince.

Mallorca Toppfotball imethibitisha mapema mwanzoni mwa mwezi huu kupitia mtandano wa kijamii wa Facebook kuwa Prince atajiunga nao kwa msimu huu wa 2017/2018.

Kituo cha Mallorca Toppfotball kilianzishwa miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuzalisha vijana wenye misingi bora ya mpira ambao watakuwa na soko kwenye ushindani wa biashara ya soka