Mbeya City yaifanyia kweli Alliance FC

Muktasari:

  • Mbeya City iliyopoteza kwa Azam FC, Simba na Mtibwa Sugar, ilifunga mabao yake kupitia kwa Victor Hangaya dakika ya 18 na Eliud Ambokile dakika ya 81. Matokeo ambayo yanawatoa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na kupanda hadi nafasi ya 17 na pointi tatu.

Dar es Salaam. Alichosema Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo kuwa baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo ugenini  watakaporudi nyumbani kwao Mbeya wataanza kushinda, kauli yake ameitekeleza.
Hii ni baada ya kuichapa Alliance FC ya Mwanza mabao 2-0, kwenye mchezo wa leo Jumapili uliopigwa Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Mbeya City iliyopoteza kwa Azam FC, Simba na Mtibwa Sugar, ilifunga mabao yake kupitia kwa Victor Hangaya dakika ya 18 na Eliud Ambokile dakika ya 81. Matokeo ambayo yanawatoa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na kupanda hadi nafasi ya 17 na pointi tatu.
Mbeya City imezipita timu za Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 18 na pointi 2, mwadui FC nafasi ya 19 na pointi moja sawa na Alliance FC iliyojikita mkiani.