Mbasha: Kwenye tuhuma mpya tena

Muktasari:

  • Akiongea na mwandishi juu ya tuhuma hizo, Mbasha alisema hapendezwi na uongo huo unaosambazwa na watu na kusema watu wanasambaza kashfa utafikiri yeye anafanya Bongo Fleva lakini yeye ni mwimbaji wa nyimbo za dini na yupo upande mwingine kabisa.

MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha hivi karibuni amedaiwa kutelekeza watoto wawili aliozaa na wanawake wawili tofauti na kwenda kwa mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha ambapo ameweka kambi huko.

Akiongea na mwandishi juu ya tuhuma hizo, Mbasha alisema hapendezwi na uongo huo unaosambazwa na watu na kusema watu wanasambaza kashfa utafikiri yeye anafanya Bongo Fleva lakini yeye ni mwimbaji wa nyimbo za dini na yupo upande mwingine kabisa.

“Sio kweli hivyo vitu ni vya uongo, nakanusha kabisa, hivi kwa nini vitu vingi vinaongelewa vya uongo! alafu mimi sipendi, huu uongo uongo ni vitu vya bongo fleva, mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelea vitu ambavyo havina faida,” alisema.

Tangu mahusiano yake na Flora kuvunjika na Flora kufunga ndoa huko Mwanza, Emmanuel amekuwa akipata kashfa za hapa na pale na baadhi ya wanawake lakini kote amekuwa akipangua tuhuma hizo.