Mbao FC wafanya walichoiahidi Simba Mwanza

Muktasari:

  • Licha ya kutangulia kupata bao Wekundu hao, Mbao haikukata tamaa na kuweza kupambana kusawazisha mabao hayo.

Mwanza.Timu ya Simba imetoshana nguvu dhidi ya Mbao FC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa jioni ya leo kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.
Licha ya kutangulia kupata bao Wekundu hao, Mbao haikukata tamaa na kuweza kupambana kusawazisha mabao hayo.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali, mabao ya Simba yalifungwa na  Shiza Kichuya dk ya 16 na James Kotei dakika 49, huku ya Mbao yakifungwa na Habibu Kiyombo na Emanuel Mvuyekule.
Katika mchezo huo pia kasi ya nyota wa Simba, Okwi na Bocco haikufurukuta mbele ya kikosi cha Mbao.