Mayanga amwibukia Rashid Mandawa

Muktasari:

  • Mayanga hakumjumuisha Mandawa kwenye kikosi chake ambacho kinategemewa kusafiri leo, Mchi 19 kwenda Algeria ambako watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao, Machi 22.

KOCHA wa Taifa Stars, Salum Mayanga amedai kumfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji wake wa zamani, Rashid Mandawa ambaye anafanya vizuri na BDF XI ya Ligi Kuu Botswana.

Mayanga hakumjumuisha Mandawa kwenye kikosi chake ambacho kinategemewa kusafiri leo, Mchi 19 kwenda Algeria ambako watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao, Machi 22.

“Mandawa ni kijana ambaye nina mfahamu vizuri, najua namna yake ya uchezaji tangu kipindi kile ambacho nikiwa kocha wake pale Mtibwa, kwa sababu nilikuwa nikimwombea ruhusa kipindi kile kutoka na kwenda kufanya majaribio nje.

“Natambua yupo kwenye kiwango bora kwa hiyo nitampa naye nafasi kwa sababu nafuatilia maendeleo yake,” alisema kocha huyo wa timu ya Taifa.

Mandawa anatesa kule Botswana akiwa na mabao 11 kwenye Ligi ya nchi hiyo kabla ya mechi ya jana dhidi ya Gaborone United.