Wenger aisusa Arsenal kwa mashabiki

Muktasari:

Wenger ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuiongoza Arsenal kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham United kwenye Uwanja wa Emirates.

London, England. Kocha Arsene Wenger amesema ameamua kuachia ngazi ili kutoa fursa kwa mashabiki kuendelea kuiunga mkono Arsenal.

Wenger ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuiongoza Arsenal kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham United kwenye Uwanja wa Emirates.

Kocha huyo aliyedumu Arsenal miaka 22, alisema anaondoka katika  klabu hiyo ili kurejesha amani baada ya hali ya hewa kuchafuka na mashabiki kutishia kutokwenda uwanjani.

Mfaransa huyo alidokeza mashabiki wanapenda furaha ya kupata ushindi, lakini timu inapofanya vibaya wanachukizwa na ndio mwanza wa kuibuka mzozo.

Wenger alisema haikuwa kazi  rahisi kutangaza kujiuzulu mwishoni mwa msimu huu kutokana na mapenzi mkubwa Arsenal, lakini ameamua kuondoka ili kulinda masilahi ya klabu.