Mashabiki wa Diamond na Zari wasubiri kauli ya Hamisa Mobeto

Muktasari:

 Hamisa Mobetto hajatoa tamko lolote ambapo watu wengi wanasubiri kwa hamu kutaka kujua juu ya baadhi ya shutuma alizotoa Diamond hasa kama ni kweli amekuwa akisababisha ugomvi kwa upande wa zari kama Diamond alivyodai.

Dar es Salaam. Tangu kuibuka kwa sakata la Diamond na Hamisa Mobetto ambalo mkali huyo wa Bongo Fleva alilitolea ufafanuzi kwenye kituo cha redio na kurusha mubashara kwenye runinga ya Clouds TV, upande wa Hamisa Mobetto hujazungumza lolote.
 Hamisa Mobetto hajatoa tamko lolote ambapo watu wengi wanasubiri kwa hamu kutaka kujua juu ya baadhi ya shutuma alizotoa Diamond hasa kama ni kweli amekuwa akisababisha ugomvi kwa upande wa zari kama Diamond alivyodai.
Kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wa Diamond na Zari wamekuwa wakieleza jambo hilo kwa mitazamo tofauti tofauti.