Mashabiki Yanga walipuka kumpokea Feisal

Dar es Salaam. Mashabiki wa Yanga umejitokeza makao makuu ya klabu hiyo kwa ajili ya kushuhudia utambulisho wa wachezaji wao wapya Feisal Salum Abdalah “FEI TOTO” na Jaffar Mohammed.

Feisal amejiunga rasmi na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar kwani kusaini jioni ya leo mkataba wa miaka mitatu.

Awali kiungo huyo aliripotiwa kujiunga na Singida United, lakini Yanga imeizidi kete kwa kumalizana na klabu yake.

Mashabiki wa Yanga wameonekana kufurahishwa na usajili huo huku wakitumia vijembe kwa watani zao,Simba kuwa wao wanasajili kwa kutumia akili.

Mara baada ya utambulisho wake rasmi mbele ya vyombo vya habari,Feisal alitoa neno kwa mashabiki hao.

"Sina mengi zaidi ya kuwaambia mashabiki wa Yanga wasubiri mambo mazuri kutoka kwangu, " alisema Feisal.

Wakati huohuo; kiungo Jaffar Mohammed amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Yanga, alisema anatarajia kufanya vizuri kama ambavyo alivyokuwa akifanya katika timu zake za nyuma.

Huu ni usajili wa tatu kwa Yanga baada ya juzi kumsainisha kiungo Mohammed Issa 'Banka'.