Mashabiki Serbia watoana ngeu uwanjani

Muktasari:

Timu hizo zinashiriki Ligi Kuu ya Serbia maaraufu SiperLiga.

Seribia. Mechi ya watani wa jadi mjini Belgrad kati ya  Red Star na Partizan imeisha kwa mkong’oto uwanjani baada ya mashabiki wa Partizan wenyewe kutofautiana kauli.

Mashabiki 17 wamejuruhiwa kutokana na ugomvi uliozuka uwanjani hapo, huku baada yao wakiwahishwa hosptitali kutokana na kuumia zaidi.

Timbwili hilo lilitokea kabla ya dakika 10 mchezo kumalizika, ambapo wachezaji wa Partizan timu moja walitofautiana wenyewe kwa wenyewe wakati wakiendelea kushangilia.

Hata hivyo, habari zilieleza kwamba chanzo cha ugomvi huo ni kutokana na matatizo ya ujinga wao wenyewe  kwani wangeweza kumaliza tofauti zao.