Mashabiki Arsenal wasusa uwanjani

Muktasari:

Zaidi ya mashabiki 30,000 wa Arsenal walikacha kwenda Emirates kushuhudia mchezo wa Kombe la Europa ambao timu hiyo ilishinda mabao 6-0 dhidi ya BATE Borisov.

LONDON, ENGLAND. Kwa mara ya kwanza mashabiki wa klabu ya Arsenal wamepungua kwenye Uwanja wa Emirates.

Zaidi ya mashabiki 30,000 wa Arsenal walikacha kwenda Emirates kushuhudia mchezo wa Kombe la Europa ambao timu hiyo ilishinda mabao 6-0 dhidi ya BATE Borisov.

Mashabiki 54,648 walijitokeza kwenye uwanja huo ikiwa ni pungufu ya watu 30,000.

“Hii ni mara ya kwanza kushuhudia idadi ndogo ya mashabiki kujitokeza kwenye Uwanja wa Emirates,” alisema mchambuzi wa soka gazeti la Dailymail.

Hata hivyo, mashabiki waliohudhuria mchezo huo waliduwazwa na mvua ya mabao iliyopata Arsenal kupitia kwa wachezaji Mathieu Debuchy, Theo Walcott, Jack Wilshere, Olivier Giroud, Mohamed Elneny na Dzyanis Palyakow aliyejifunga.