Mashabiki wa AC Milan wamtimua Gianluigi

Muktasari:

Mashabiki wamtamkia kuwa uvumilivu wao umefika kikomo kuhusu uamuzi wake wa kutishia kutaka kuondoka klabuni hapo.

Italia. Kipa wa AC Milan amesema amembiwa  akatishe mkataba wake na klabu hiyo, huku mashabiki wakimuwashia moto kwamba aondoke tu.

Mchezaji huyo mwenye miaka 18, alisaini mkataba mpya msimu uliopita wa kiangazi lakini, katika mchezo wa AC Milan dhidi ya Verona walioibuka na ushindi wa mabao 3-0. Mashabiki wa AC Milan uwanjani hapo, walipeperesha bendera wakimtaka aondoke klabuni hapo na kueleza kuwa wamefikia kikomo kumvumilia.

Nahodha wa timu hiyo, Leonardo Bonucci ampa moyo kutokana na mashabiki hao kumgeuzia kibao wakati wa mechi hiyo.