Masau Bwile awashangaa Kagera kushangilia sare

Monday September 11 2017

 

By Olipa Assa

Kagera Sugar na Ruvu Shooting, zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, Uwanja wa Kaitaba uliyopo Mwanza, ndipo msemaji wa wavaa magwanda, Masau Bwile, akacheka na kuwashangaa wapinzani wao kushangilia sare.

Bwile amesema timu yao ilitawala mchezo, hivyo Kagera hawakuamini baada ya kusawazisha dakika za mwisho na kushangilia kana kwamba wao ndiyo wamecheza ugenini.

"Tunapowaambia Ruvu ni timu yenye majembe yanayojua kufanya kazi popote lazima wadau waliheshimu hilo, unaona sasa yaliyotaka kuwakuta Kagera hadi wanashangilia sare, wakati sisi tulikuwa tunasaka pointi tatu," anasema.