Manyika aisubiri Simba

Saturday January 13 2018

 

By Oliver Albert

Dar es Salaam.Kipa wa Singida United,Manyika Peter amesema mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu kutokana na uimara wa wapinzani wao.
Singida United itacheza na Simba Alhamis ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salamaa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Timu hiyo ambayo ilitolewa na Azam katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, imeanza kuivutia kasi Simba jana Ijumaa katika mazoezi yaliyofanyika katika fukwe za Aghakan Posta.
Manyika msimu uliopita alikuwa akiichezea Simba amekiri mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani utakuwa mgumu, lakini wanajipanga kuondoka na pointi zote tatu.
"Itakuwa mechi ngumu kwani wapinzani wetu ni moja ya timu nzuri, hivyo inabidi tujipange hasa. Tunaendelea kujiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri.
"Tuna kikosi kizuri na tunafurahia mwenendo wetu kwenye ligi hivyo lazima tuhakikishe hata mchezo huo dhidi ya Simba tunashinda.Uwezo wa kushinda tunao hivyo hatuna hofu yoyote.