Manchester City yamsajili beki wa Real Madrid

Muktasari:

  • Mchezaji huyo kimataifa raia wa Brazil, amekula shavu hilo kwa mkataba wa miaka mitano na ataungana na kikosi hicho kwenye mechi za maandalizi msimu huu nchini Marekani.

England. Klabu ya Manchester City imemsajili beki wa Real Madrid, Danilo kwa gharama ya Pauni 26.5 milioni.

Mchezaji huyo kimataifa raia wa Brazil, amekula shavu hilo kwa mkataba wa miaka mitano na ataungana na kikosi hicho kwenye mechi za maandalizi msimu huu nchini Marekani.

Danilo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na klabu hiyo kwenye usajili wa msimu huu wa kiangazi, huku ikielezwa ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi ya beki na kiungo.