Neymar apewa jukumu zito kikosi cha Brazil Kombe la Dunia

Wednesday May 16 2018

 

By EVAGREY VITALIS

Neymar, 26, alifanyiwa upasuaji mwezi Machi. Awali, daktari wa timu ya Taifa ya Brazil alisema hataweza kucheza kwa miezi mitatu.

Wachezaji wanne wanaocheza Manchester City Ederson, Danilo, Fernandinho na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaosakatia gozi Ligi ya Premia ambao wamo kwenye kikosi hicho.

Wengine ni nyota wa Liverpool Roberto Firmino na winga wa Chelsea Willian.

Beki wa kulia wa PSG Dani Alves atakosa michuano hiyo baada ya kupata jeraha la goti wiki iliyopita.

Brazil wamo Kundi E na Costa Rica, Serbia na Uswizi na watacheza mechi yao ya kwanza Jumapili 17 Juni.