Manchester City wamzingua Nolito, wamrudisha Hispania

Friday July 21 2017

 

London, England. Nolito aliyepo England anakaribia kutimka baada ya klabu za Manchester City na Sevilla kufikia mwakafa wa ada ya Pauni 8 milioni kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji huyo.

Raia huyo wa Hispania anatarajiwa kwenda Sevilla ili kumbadili Vitolo anayetajwa kutimkia Atletico Madrid.

Miongoni mwa wachezaji ambao kocha Pep Guadiola aliwaongeza katika simu wa kiangazi msimu wa 2016/2017 alikuwa ni Nolito.Hata hivyo alishindwa kuonyesha ubora wake kwenye dimba la Etihad baada ya kufunga mabao matano tu katika msimu wote, huku akizidiwa kiwango na Leroy Sane na Raheem Sterling ambao wamejihakikishia nafasi za ushambuliaji.