Man City yapanga kufunga usajili kwa kumsajili Sanchez

Muktasari:

  • Kocha Pep Guardiola anafanya kila liwezekanalo kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi huu.

Manchester City inatuma ofa ya mwisho ya Pauni 60 milioni kwa klabu ya Arsenal ili kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez, kwa mujibu wa taarifa.

Kocha Pep Guardiola anafanya kila liwezekanalo kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi huu.

Sanchez yupo katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na Arsenal, huku kocha Arsene Wenger ikisisitiza kuwa mchezaji huyo hatauzwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph, suala hilo linaonekana kuwa gumu kuishawishi Arsenal kumuuza, huku ikijiandaa kumpa Sanchez ofa ya mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki kama atakubali kutua Etihad.