Man City yaibania Arsenal

Man City yaibania MANCHESTER City imemwambia Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger asahau kumnasa staa, Raheem Sterling na wamepanga kumpa mkataba mpya staa huyo licha ya mkataba wake wa sasa kubakiza miaka mitatu.

Wenger anamtaka staa huyo atumike kama chambo endapo City itataka kumchukua staa wake wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez katika dirisha la Januari lakini City inataka kumfunga zaidi klabuni hapo.