Mambo matano yakuvutia Yanga, Gor Mahia

Muktasari:

  • Yanga inahitaji ushindi ili kurudisha matumaini yake ya kusonga mbele katika kundi hilo

Nairobi. Habari ya Mjini hapa Nairobi ni mechi kali kati ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya Gor Mahia dhidi ya Yanga katika mechi ya Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wanaingia katika mechi ya kesho wakiburuza mkia na  pointi moja baada ya kutoka suruhu na Rayon Sport baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa USM Alger.

Wakati Gor Mahia wao wanapointi mbili baada ya kutoka sare mechi zote mbili dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na USM Alger ya Algeria.

Katika mechi ya kesho Jumatano ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Kasarani saa 1:00 usiku kulingana na presha ilivyo huenda kuna mambo yakatokeo.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo matano ambayo huenda yakajitokeza katika mechi ya Gor Mahia dhidi ya.

 

Yanga kushtukiza

Kulingana na kikosi cha Yanga kukosekana baadhi ya nyota wao wa kikosi cha kwanza kama Kelvin Yondani, Hassan Kessy na wengine hawatakuwa wakimilika mpira muda mwingi.

Yanga watakuwa wakishambulia zaidi kwa kushtukiza tena kwakupitia pembeni ambapo kutakuwa na mawinga Godfrey Mwashuiya, Juma Mahadhi na Emmanuel Martine.

Muda mwingi tutakuwa tukishuhudia Gor Mahia wakimiliki mpira wakati Yanga wao wakifanya mashambulizi ya kushtukiza na kama wakiwa makini wanaweza kufunga bao kupitia njia hiyo.

Mabao ya kutosha

Kulingana na kila timu kuamini kuwa inaweza kumfunga mwenzake mechi inaweza ikamalizika  na matokeo ya mabao mengi.

Yanga wao wanaamini kuwa hii ndio mechi yao ya kwanza kushinda wakati Gor Mahia wanaamini hivyo na sababu kubwa kuzifunga Singida United, Simba ambazo zinatokea Tanzania.

Yanga kuamua mechi

Mabeki wa Yanga ni wazi watacheza kulia atakuwa Juma Abdul, kushoto Gadiel Michael na wale wa kati ni Adrew Vicent na Abdallah Shaibu ndio watakuwa na jukumu la kuamua mechi.

Ni wazi Gor Mahia wapo vizuri katika kushambulia wakiongozwa na Jacques Tuyisenge na Francis Kahata ambaye amekuwa akiwindwa vikali na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba.

Mabeki wa Yanga wataweza kuwazuia washambuliaji wa Gor Mahia kutokufanya mazara langoni mwao watamaliza dakika tisini kufua mbele, lakini wakiwa wanafanya makosa ya mara kwa mara ni wai wataondoka mikono nyuma.

Ubora wa Rostand

Mahala pengine ambapo Yanga watafanikiwa kuondoka na pointi tatu hapa Nairobi katika mechi na Gor Mahia ni kipa wao namba moja Youth Rostand amekuwa na makosa mengi.

Rostand ni wazi ndio ataanza katika mechi ya kesho, lakini amekuwa na makosa mengi na kuighalimu timu haswa katika mipira ya krosi imekuwa ikimsumbua sana.

Gor Mahia ni wazuri katika kuruka vichwa si washambuliaji bali hata mabeki katika mipira ya adhabu na kama Rostand atakuwa ameyafanyia kazi matatizo hayo wataaliza mechi salama.

Yanga viungo watatu

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera hatakuwepo katika benchi la ufundi kwa sababu bado hajatimiza vibali vyake vya kazi huenda akaanzisha viungo wa tatu ili kuanza kukaba kwanza.

Viungo Papy Tshishimbi, Juma Makapu na Pius Buswita wakawa katika kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Gor Mahia na lengo likiwa ni kujilinda kwanza maana wanacheza ugenini.

Yanga wamezoeleka kuwa bora katika kushambulia kupitia pembeni kama wakianza hivi huenda wakafanikiwa katika kuzua, lakini wakashindwa kwenye kushambulia.

Ni wazi kiungo mmoja atakwenda kucheza kama winga jambo hatakuwa na sifa za winga kama kupiga krosi, kushambulia kwa haraka kama Zahera anavyotaka.