Makipa wa Yanga Kakolanya na Rostand ngoma droo

Muktasari:

  • Alisema kuwa ujio wa kipa huyo unazidi kutanua wigo wa kikosi chao lakini pia kunafanya kuwa na kikosi imara ambacho mchezaji yeyote akikosekana basi kunakuwa hakuna wasiwasi wowote.

Kipa Beno Kakolanya wa Yanga amefunguka kuwa ujio wa kipa Youthe Rostand katika kikosi chao kunazidi kufanya klabu hiyo kuongeza nguvu ya kusaka ushindi kutokana na umahiri aliokuwa nao.

Alisema kuwa ujio wa kipa huyo unazidi kutanua wigo wa kikosi chao lakini pia kunafanya kuwa na kikosi imara ambacho mchezaji yeyote akikosekana basi kunakuwa hakuna wasiwasi wowote.

Akizungumzia ushindani wa namba kati yao alisema kuwa hafikirii kama kutakuwa na ushidani kati yao, badala yake watakuwa wakipambania timu yao kuweza kufanya vizuri katika kutafuta ubingwa kwenye makombe wanayoshiriki.

Kakolanya aliongea kuwa afya yake imeanza kuimarika baada ya kupata matibabu na  kuwa na muda wa wa kutosha ili kupumzika hivyo anasubilia ruhusa kutoka kwa daktari ili aweze kujiunga na wenzake katika maandalizi ya Ligi Kuu.