Makapu, Buswita hawasomeki Yanga

Muktasari:

  • Kocha Zahera amekuwa akitilia mkazo suala la nidhamu kwa wachezaji wake hasa katika kipindi hiki

Dar es Salaam. Yanga itawakosa wachezaji wake Said Makapu, Ramadhan Kabwili, Juma Abdul na Pius Buswita, katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union.

Makapu, Kabwili na Buswita wameondolewa kambini kwa makossa ya utovu wa nidhamu, ambapo kocha mkuu Mwinyi Zahera alifikia uamuzi huo ili kulinda heshima katika kikosi chake.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema wachezaji hao wameondolewa kutokana na mwalimu kuendelea kulinda nidhamu katika klabu yao.

"Mwalimu wetu anataka kulinda heshima ndani ya klabu yetu kwahiyo hapendi mambo ya tofauti, tutawakosa katika mchezo huu na kuna adhabu watapewa wakirejea, lakini hatuwezi kuziweka hivi sasa nje ni ndani kwa ndani," alisema.

Aliongeza kwamba timu hiyo itaendelea kumkosa winga wao Juma Mahadhi anayesumbuliwa na maumivu ya goti.