Majaliwa awasaka Yanga uzinduzi Copa Umisseta

Muktasari:

  • Waziri mkuu Majaliwa ambaye ni shabiki wa Simba katika hotuba yake alijikuta akihoji hivi viongozi wa Yanga nao wapo hapa uwanjani kusaka vipaji? Kauli ambayo ilionekana kuwafurahisha maelfu ya wadau wa michezo walioshiriki kwenye hafla hiyo.

Mwanza. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliamua kuwachekesha mashabiki wa soka kwa kuhoji uwepo wa Yanga katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Coca cola Umisseta leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Waziri mkuu Majaliwa ambaye ni shabiki wa Simba katika hotuba yake alijikuta akihoji hivi viongozi wa Yanga nao wapo hapa uwanjani kusaka vipaji? Kauli ambayo ilionekana kuwafurahisha maelfu ya wadau wa michezo walioshiriki kwenye hafla hiyo.

"Taarifa nilizonazo ni kwamba viongozi wa Simba wako hapa uwanjani kuangalia vipaji, Azam pia wako hapa nadhani hata Yanga watakuepo, eti jamani Yanga nao si wapo?," alihoji Waziri mkuu kwa utani.

Katika ufunguzi huo Waziri mkuu alirusha mpira wa kikapu kwa ishara ya kutosi na kupuliza kipenga kwenye soka kuashiria ufunguzi huo.