Madrid bila Ronaldo mbona itasonga sana tu- Garcia

Sergio Garcia 

Muktasari:

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuwapo tetesi za kuondoka klabuni hapo tangu wiki iliyopita.

Hispania. Sergio Garcia amesema mabingwa wa Ulaya na Hispania, Real Madrid watasonga mbele zaidi hata kama Cristiano Ronaldo ataondoka.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuwapo tetesi za kuondoka klabuni hapo tangu wiki iliyopita.

Hata hivyo, rais wa klabu hiyo, Florentino Perez tayari ametoa uamuzi kuwa mchezaji huyo haondoki, huku Garcia akisisitiza kwamba klabu hiyo itaendelea kufanya vyema hata kama mchezaji huyo mwenye miaka 32 akiondoka klabuni.

Alisema huenda mashabiki wa Real Madrid wakahuzunika kuondokewa na mchezaji ambaye ni bora, lakini akiamini kwamba bado kikosi hicho hakitatetereka.

Ronaldo amefunga mabao 40 katika mashindano yote aliyocheza na mabao 25 kati ya hayo amefunga kwenye mechi za La Liga.