Madini yasuka kikosi upya

Muktasari:

Madini inayojiandaa na Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza kucheza michezo ya kirafiki wiki ijayo tayari kujianda na msimu mpya.

Arusha: Kocha wa Madini Sc, Abdalah Juma amesema anategemea kuunda kikosi chake kikiwa na sura mpya nyingine msimu ujao.

Madini inayojiandaa na Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza kucheza michezo ya kirafiki wiki ijayo tayari kujianda na msimu mpya.

“Tumeingiza sura mpya ya wachezaji 25 kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Arusha, wengine walishiriki Ligi Kuu miaka ya nyuma na wengine tumewapandisha kutoka timu yetu ya vijana,” alisema Juma.

Madini imewaacha wachezaji wanne, wengine wakiwa wameondoka baada ya kumaliza

mikataba yao akiwemo kiungo aliyeng’aa Awesu Awesu na kipa namba moja Ramadhan

Chalamanda