Madeni, namba vyamkimbiza Beno Yanga

Muktasari:

  • Kipa huyo tangu kuanza kwa msimu huu hajawa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao.

Siku za kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kubaki katika timu hiyo zimeanza kuhesabika baada ya kushindwa kulipwa madai yake.

Kw mujibu wa Meneja, Seleman Haroub alisema sababu ya kipa huyo kutaka kuondoka ni kutomaliziwa pesa yake ya usajili pamoja na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

"Ni kweli natambua kuna wakati klabu inaweza kupitia kwenye wakati mgumu, ndiyo maana siwezi kulalamikia juu ya mshahara najua kila mchezaji anaweza akacheleweshewa, tatizo ni kutomaliziwa pesa ya usajili,"alisema Haroub.

Haroub alisema kikao hicho kitatoa taswira kama mteja wake anaweza akaendelea na Wanajangwani ama kuondoka kwa madai bado ana mkataba wa miezi saba.

"Hii ni kazi na ina makubaliano maalum, lazima nifuatilie kwa nini wapo kimya na hawasemi lolote kama watamlipa lini ili hata yeye apate moyo,la mtajua badae anakwenda wapi,"alisema huku Yanga jana wakiwa kimya kwa kutokataka kufafanua sakata hilo.