Madee amtuliza Nay Wa Mitego

Muktasari:

  • Katika mahojiano na mwandishi, Madee aliulizwa juu ya bifu lao kama limeisha ama laah.
  • “Sina bifu na Nay na wala siwezi kuwa na bifu nae ni kutofautiana tu kauli lakini pia mi niwe na bifu na Nay, mbona mtoto mdogo sana kwangu.”

Dar es Salaam. Pengine unaweza kufikiri bifu lao limeisha kutokana na wao wanavyodai lakini kutokana na maneno wanayoongea wote wawili hali inaonekana bado si nzuri.

Katika mahojiano na mwandishi, Madee aliulizwa juu ya bifu lao kama limeisha ama laah.

“Sina bifu na Nay na wala siwezi kuwa na bifu nae ni kutofautiana tu kauli lakini pia mi niwe na bifu na Nay, mbona mtoto mdogo sana kwangu.”

“Mimi wakati natoa wimbo wangu wa kwanza yeye sijui alikuwa yupo sekondari hata sijui, kwa hiyo siwezi kuwa na bifu na mtoto mdogo kabisa,” aliongeza.

Pia Madee alijibu shutuma ambayo imewahi kutolewa na Jackline Wolper juu ya video ya Sikila ambapo Wolper alidai Madee kutumia sura yake bila idhini yake.

“Unajua suala la katuni ni suala ambalo ni kama la kubuni tu, haimaanishi kwamba ndo sura halali ya mtu fulani,sasa mimi nilishangaa kwa alichokisema lakini yote na yote nshukuru mambo yalienda safi,” alisema Madee.