Mabingwa wa soka Karatu wapewa kombe lao

Muktasari:

Timu hiyo imemaliza ligi kwa kuifunga  Beach Boys kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Bondeni

Karatu:  Mabingwa wapya wa soka wilaya ya Karatu, Bougainvillia Fc wamekabidhiwa kombe lao na kutakiwa kuanza maandalizi mapema ya ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Arusha.

Timu hiyo imemaliza ligi kwa kuifunga  Beach Boys kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Bondeni na kufikisha pointi 12, huku wakiwa wanasubili mchezo wa leo jioni kati ya Bashay Fc na Generation Fc uliomalizika kwa Bashay kushinda mabao 2-1.

Mabao ya Bougainvillia yalifungwa na Mohammed Pachaa aliyefunga mabao matatu huku John Chuguna na James Aulerian waliotupia kila mmoja bao moja moja.

Ligi ya Karatu ilishirikisha timu sita pekee timu nyingine ni Kifaru Fc na Viwawa Fc, huku Katibu wa Chama cha soka wilayani humo Kelvin Hamis akisema timu nyingi zilikwepa kulipa ada ya aliyokuwa Sh150,000.

Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Waziri Morice alisema vijana wengi wanashindwa kuendelea kutokana na makundi mabaya wanayofuata bila kutathimini mwisho wake.

Aliongeza kuwa ili kuimalish Michezo wilayani humo ataanzisha ligi mwezi Oktoba itakayoitwa kurugenzi cup na bingwa atajinyakulia kumbe na laki tano.