Cannavaro, Kessy wapishana Kiswahili

Muktasari:

  • Yanga wamefika mjini Shinyanga leo Ijumaa tayari kwa maandalizi ya mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Stand United.

Mabeki wa Yanga, nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Hassan Kessy wamedaiwa kutaka kuzichapa baada ya kupishana Kiswahili kwenye ya mazoezi ya timu yao jana Alhamisi mjini Tabora.

Chanzo cha habari kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa, wachezaji hao nusura wazichape mara baada ya mazoezi hayo yaliyofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kabla ya kuelekea mjini Shinyanga.

Awali zilizagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wawili hao walishikana mashati, lakini mmoja ya wachezaji wa timu hiyo (jina kapuni), alikiri Cannavaro na Kessy walitofautiana kauli na kutupiana maneno kabla ya kuamuliwa.

“Ni kweli jamaa walizinguana kidogo kwa maneno, lakini walimazana kiungwana na kwa sasa tupo Shinyanga tukijiandaa na mchezo wetu wa kesho na Stand United tukiwa freshi,” alisema mchezaji huyo.