Mabao 300, PSG, Ronaldo habari nyingine

Thursday December 7 2017

 

London, England. Jumla ya mabao 306 yamefungwa katika hatua ya makundi ikiwa ni rekodi mpya katika historia ya Ligi ya Mabingwa, huku Cristaano Ronaldo akiongoza katika orodha ya ufungaji.

Katika mabao hayo klabu zilizofunga magoli mengi zaidi ni Paris Saint-Germain iliyofunga mabao 25 katika mechi sita wakifuatiwa na Liverpool (23), na Real Madrid (21) katika idadi ya jumla ya magoli 306 yaliyofungwa katika mechi 96 za hatua ya makundi.

PSG imeweka rekodi ya kuwa timu iliyofunga mabao mengi zaidi katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wakifuatiwa na Liverpool iliyoshinda 7-0 dhidi ya Spartak Moscow katika mchezo wa hatua ya makundi. 

Wakati klabu hiyo zikiweka rekodi hiyo, mfungaji bora wa msimu uliopita Ronaldo aliyefunga mabao 12 na kuiwezesha Real kutetea ubingwa wake kwa sasa pia anaongoza akiwa amefunga mabao tisa baada ya kucheza mechi sita.

Wanaofuatia Ronaldo kwa karibu wakiwa wamefunga mabao sita ni mshambuliaji  Tottenham Spurs, Harry Kane akiwa pamoja na nyota wa Paris Saint-Germain, Neymar na Edinson Cavani, wengine ni mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino pamoja na Wissam Ben Yedder (Sevilla).

 

1

Cristiano Ronaldo

Real Madrid

9

=2

Neymar

PSG

6

=2

Harry Kane

Tottenham

6

=2

Edinson Cavani

PSG

6

=2

Wissam Ben Yedder

Sevilla

6

=2

Roberto Firmino

Liverpool

6

=7

Philippe Coutinho

Liverpool

5

=7

Mohamed Salah

Liverpool

5

=7

Vincent Aboubakar

Porto

5

=10

Cenk Tosun

Besiktas

4

=10

Raheem Sterling

Manchester City

4

=10

Dimitri Oberlin

Basel

4

=10

Kylian Mbappe

PSG

4

=10

Romelu Lukaku

Manchester United

4

=10

Anderson Talisca

Besiktas

4

=10

Pierre-Emerick Aubameyang

Borussia Dortmund

4