MO Ibrahim arudishwa kikosi cha kwanza Simba

Muktasari:

Simba imeshinda mechi zake mbili za kwanza za Ligi Kuu Bara msimu huu

Mtwara. Hatimaye kiungo Mohammed Ibrahim 'MO Ibra' amerudi katika kikosi cha kwanza Simba baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Mo Ibrahimu alionyesha kiwango cha juu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard na kufunga bao mmoja kimemfanya kocha wake Patrick Aussem kumwamini kwa mara ya kwanza.

MO Ibra hajacheza mechi mbili za kwanza za Ligi kuu ambazo Simba walicheza dhidi ya Tanzania Prison na Mbeya City alikuwa katika benchi la wachezaji wa akiba.

Ibrahimu anaanza katika kikosi cha kwanza katika nafasi ya Hassan Dilunga ambaye alicheza mechi zote tatu za kimashindano ambazo Simba walicheza msimu huu.

MO Kama atacheza katika kiwango kizuri katika mechi hii huenda akamtia njaa Dilunga ambaye ni majeruhi wa goti au Cletus Chama ambaye yupo katika benchi la wachezaji wa akiba.

Kama MO atacheza na kuchoka ni wazi mabadiliko yake ataingia Chama ambaye alitua jana Ijumaa hapa Mtwara akitokea nchini Gambia ambapo timu yake ya Taifa ya Zambia ilicheza mechi huko.

Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim, John Bocco, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere.